Matendo 15:38
Acts 15:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Paulo aliona si vyema kwa sababu aliwahi kuwaacha walipokuwa huko Pamfilia, hakutaka kuendelea kufanya kazi naye.
Acts 15:38 in English
Acts 15:38 · Berean Standard Bible
But Paul thought it best not to take him, because he had deserted them in Pamphylia and had not accompanied them in the work.
Context
36Baada ya muda, Paulo akamwambia Barnaba, “Turudi tukawatembelee ndugu katika miji yote tuliyohubiri neno la Bwana tuone jinsi wanavyoendelea.” 37Barnaba alitaka wamchukue Yohana aitwaye Marko waende naye. 38Lakini Paulo aliona si vyema kwa sababu aliwahi kuwaacha walipokuwa huko Pamfilia, hakutaka kuendelea kufanya kazi naye. 39Pakatokea ubishi mkali kati ya Paulo na Barnaba kuhusu jambo hili, hivyo wakagawanyika. Barnaba akamchukua Yohana Marko wakasafiri baharini kwenda Kipro. 40Lakini Paulo akamchagua Sila na akaondoka baada ya ndugu kuwatakia neema ya Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.