3 Yohana 1:4
3 John 1:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sina furaha kubwa kuliko hii, kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli.
3 John 1:4 in English
3 John 1:4 · Berean Standard Bible
I have no greater joy than to hear that my children are walking in the truth.
Context
2Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza juu ya uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli. 4Sina furaha kubwa kuliko hii, kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli. 5Rafiki mpendwa, wewe ni mwaminifu kwa yale unayowatendea ndugu, ingawa wao ni wageni kwako. 6Wameshuhudia kuhusu upendo wako mbele ya kanisa. Utafanya vyema ukiwasafirisha kama inavyostahili kwa Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.