2 Wathesalonike 1:4
2 Thessalonians 1:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndiyo sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.
2 Thessalonians 1:4 in English
2 Thessalonians 1:4 · Berean Standard Bible
That is why we boast among God’s churches about your perseverance and faith in the face of all the persecution and affliction you are enduring.
Context
2Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo iwe nanyi. 3Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka. 4Ndiyo sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili. 5Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa Ufalme wa Mungu, mnaoteswa kwa ajili wake. 6Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wawatesao ninyi
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.