2 Wathesalonike 1:3
2 Thessalonians 1:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka.
2 Thessalonians 1:3 in English
2 Thessalonians 1:3 · Berean Standard Bible
We are obligated to thank God for you all the time, brothers, as is fitting, because your faith is growing more and more, and your love for one another is increasing.
Context
1Paulo, Silvano* na Timotheo:
Kwa kanisa la Wathesalonike mlio katika Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo: 2Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo iwe nanyi. 3Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka. 4Ndiyo sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili. 5Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa Ufalme wa Mungu, mnaoteswa kwa ajili wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.