2 Samweli 3:6
2 Samuel 3:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati wa vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi, Abneri alikuwa anajiimarisha katika nafasi yake kwenye nyumba ya Sauli.
2 Samuel 3:6 in English
2 Samuel 3:6 · Berean Standard Bible
During the war between the house of Saul and the house of David, Abner had continued to strengthen his position in the house of Saul.
Context
4wa nne, Adoniya mwana wa Hagithi;
wa tano, Shefatia mwana wa Abitali; 5wa sita, Ithreamu mwana wa Egla, mkewe Daudi.
Hawa ndio waliozaliwa kwa Daudi huko Hebroni. 6Wakati wa vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi, Abneri alikuwa anajiimarisha katika nafasi yake kwenye nyumba ya Sauli. 7Basi Sauli alikuwa amekuwa na suria, jina lake Rispa binti wa Aiya. Naye Ish-Boshethi akamwambia Abneri, “Kwa nini umekutana kimwili na suria wa baba yangu?” 8Abneri akakasirika sana kwa sababu ya kile Ish-Boshethi alichosema, naye akamjibu, “Je, mimi ni kichwa cha mbwa, kwa upande wa Yuda? Siku hii ya leo mimi ni mtiifu kwa nyumba ya baba yako Sauli, kwa jamaa yake na rafiki zake. Sijakukabidhi kwa Daudi, lakini bado unanilaumu kwa kosa la kuhusika na huyu mwanamke!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.