2 Samweli 22:5
2 Samuel 22:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea.
2 Samuel 22:5 in English
2 Samuel 22:5 · Berean Standard Bible
For the waves of death engulfed me; the torrents of chaos overwhelmed me.
Context
3Mungu wangu ni mwamba wangu,
ambaye kwake ninakimbilia,
ngao yangu na pembe ya wokovu wangu.
Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu
na mwokozi wangu,
huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri. 4Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa,
nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. 5“Mawimbi ya mauti yalinizunguka,
mafuriko ya maangamizi yalinilemea. 6Kamba za kuzimu* zilinizunguka,
mitego ya mauti ilinikabili. 7Katika shida yangu nalimwita Bwana,
nilimlilia Mungu wangu.
Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu,
kilio changu kikafika masikioni mwake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.