2 Samweli 2:17
2 Samuel 2:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Siku hiyo vita vilikuwa vikali sana, naye Abneri na watu wa Israeli wakashindwa na watu wa Daudi.
2 Samuel 2:17 in English
2 Samuel 2:17 · Berean Standard Bible
The battle that day was intense, and Abner and the men of Israel were defeated by the servants of David.
Context
15Kwa hiyo vijana wakasimama, wakahesabiwa: watu wa Benyamini na wa Ish-Boshethi mwana wa Sauli kumi na wawili, na upande wa Daudi kumi na wawili. 16Kisha kila mtu akakamatana na mpinzani wake kichwani na kuchomana kwa upanga, nao wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale katika Gibeoni pakaitwa Helkath-Hasurimu.* 17Siku hiyo vita vilikuwa vikali sana, naye Abneri na watu wa Israeli wakashindwa na watu wa Daudi. 18Wana watatu wa Seruya walikuwako huko: nao ni Yoabu, Abishai na Asaheli. Basi huyo Asaheli alikuwa na mbio kama paa. 19Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.