Native Bible

2 Samuel 2:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata.

2 Samuel 2:19 in English

2 Samuel 2:19 · Berean Standard Bible

and he chased Abner, not turning to the right or to the left in his pursuit.

Context

17Siku hiyo vita vilikuwa vikali sana, naye Abneri na watu wa Israeli wakashindwa na watu wa Daudi. 18Wana watatu wa Seruya walikuwako huko: nao ni Yoabu, Abishai na Asaheli. Basi huyo Asaheli alikuwa na mbio kama paa. 19Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata. 20Abneri akaangalia nyuma na kumuuliza, “Ni wewe, Asaheli?” Akamjibu, “Ndiyo.” 21Ndipo Abneri akamwambia, “Geuka upande wa kulia au kushoto. Mchukue mmoja wa vijana wa kiume na umvue silaha zake.” Lakini Asaheli hakuacha kumfukuza.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.