2 Samweli 2:18
2 Samuel 2:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wana watatu wa Seruya walikuwako huko: nao ni Yoabu, Abishai na Asaheli. Basi huyo Asaheli alikuwa na mbio kama paa.
2 Samuel 2:18 in English
2 Samuel 2:18 · Berean Standard Bible
The three sons of Zeruiah were there: Joab, Abishai, and Asahel. Now Asahel was fleet of foot like a wild gazelle,
Context
16Kisha kila mtu akakamatana na mpinzani wake kichwani na kuchomana kwa upanga, nao wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale katika Gibeoni pakaitwa Helkath-Hasurimu.* 17Siku hiyo vita vilikuwa vikali sana, naye Abneri na watu wa Israeli wakashindwa na watu wa Daudi. 18Wana watatu wa Seruya walikuwako huko: nao ni Yoabu, Abishai na Asaheli. Basi huyo Asaheli alikuwa na mbio kama paa. 19Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata. 20Abneri akaangalia nyuma na kumuuliza, “Ni wewe, Asaheli?”
Akamjibu, “Ndiyo.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.