2 Samweli 1:5
2 Samuel 1:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Daudi akamwambia huyo kijana aliyemletea taarifa, “Je, umefahamuje kwamba Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?”
2 Samuel 1:5 in English
2 Samuel 1:5 · Berean Standard Bible
Then David asked the young man who had brought him the report, “How do you know that Saul and his son Jonathan are dead?”
Context
3Daudi akamuuliza, “Wewe umetoka wapi?”
Akamjibu, “Nimetoroka kutoka kambi ya Waisraeli.” 4Daudi akamuuliza, “Ni nini kilichotokea? Niambie.”
Akasema, “Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wao walianguka na kufa. Naye Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa.” 5Ndipo Daudi akamwambia huyo kijana aliyemletea taarifa, “Je, umefahamuje kwamba Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?” 6Yule kijana akasema, “Nilijipata huko Mlima Gilboa, naye Sauli alikuwa huko akiegemea mkuki wake, na magari ya vita na wapanda farasi wa upande wa adui wakawa wamemkaribia sana. 7Alipogeuka na kuniona, akaniita, nami nikasema, ‘Je, nifanye nini?’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.