Native Bible

2 Samuel 1:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Alipogeuka na kuniona, akaniita, nami nikasema, ‘Je, nifanye nini?’

2 Samuel 1:7 in English

2 Samuel 1:7 · Berean Standard Bible

When he turned around and saw me, he called out and I answered, ‘Here I am!’

Context

5Ndipo Daudi akamwambia huyo kijana aliyemletea taarifa, “Je, umefahamuje kwamba Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?” 6Yule kijana akasema, “Nilijipata huko Mlima Gilboa, naye Sauli alikuwa huko akiegemea mkuki wake, na magari ya vita na wapanda farasi wa upande wa adui wakawa wamemkaribia sana. 7Alipogeuka na kuniona, akaniita, nami nikasema, ‘Je, nifanye nini?’ 8“Akaniuliza, ‘Wewe ni nani?’ “Nikamjibu, ‘Mimi ni Mwamaleki.’ 9“Kisha akaniambia, ‘Nikaribie mimi na uniue! Niko katika maumivu makali ya kifo, lakini bado ningali hai.’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.