2 Samweli 1:3
2 Samuel 1:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Daudi akamuuliza, “Wewe umetoka wapi?” Akamjibu, “Nimetoroka kutoka kambi ya Waisraeli.”
2 Samuel 1:3 in English
2 Samuel 1:3 · Berean Standard Bible
“Where have you come from?” David asked. “I have escaped from the Israelite camp,” he replied.
Context
1Baada ya kifo cha Sauli, Daudi alipokuwa amerudi kutoka kuwashinda Waamaleki, Daudi alikaa siku mbili huko Siklagi. 2Siku ya tatu akaja mtu mwenye nguo zilizoraruka na mavumbi kichwani mwake kutoka kwenye kambi ya Sauli. Alipomjia Daudi, akajitupa chini ili kumpa heshima. 3Daudi akamuuliza, “Wewe umetoka wapi?”
Akamjibu, “Nimetoroka kutoka kambi ya Waisraeli.” 4Daudi akamuuliza, “Ni nini kilichotokea? Niambie.”
Akasema, “Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wao walianguka na kufa. Naye Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa.” 5Ndipo Daudi akamwambia huyo kijana aliyemletea taarifa, “Je, umefahamuje kwamba Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.