2 Wakorintho 10:5
2 Corinthians 10:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo,
2 Corinthians 10:5 in English
2 Corinthians 10:5 · Berean Standard Bible
We tear down arguments and every presumption set up against the knowledge of God; and we take captive every thought to make it obedient to Christ.
Context
3Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, 5tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo, 6tena tukiwa tayari kuadhibu kila tendo la kutotii, kutii kwenu kutakapokamilika. 7Angalieni yale yaliyo machoni penu. Kama mtu yeyote anaamini kuwa yeye ni mali ya Kristo, basi kumbuka kuwa kama ulivyo wa Kristo, vivyo hivyo na sisi ndivyo tulivyo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.