Native Bible

2 Corinthians 10:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo.

2 Corinthians 10:3 in English

2 Corinthians 10:3 · Berean Standard Bible

For though we live in the flesh, we do not wage war according to the flesh.

Context

1Basi, mimi Paulo ninawasihi kwa unyenyekevu na upole wa Kristo, mimi niliye “mwoga” ninapokuwa pamoja nanyi ana kwa ana, lakini mwenye ujasiri nikiwa mbali nanyi! 2Nawaomba nitakapokuja kwenu nisiwe na ujasiri dhidi ya watu fulani, kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata namna ya ulimwengu huu. 3Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, 5tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.