2 Wakorintho 10:6
2 Corinthians 10:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
tena tukiwa tayari kuadhibu kila tendo la kutotii, kutii kwenu kutakapokamilika.
2 Corinthians 10:6 in English
2 Corinthians 10:6 · Berean Standard Bible
And we will be ready to punish every act of disobedience, as soon as your obedience is complete.
Context
4Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, 5tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo, 6tena tukiwa tayari kuadhibu kila tendo la kutotii, kutii kwenu kutakapokamilika. 7Angalieni yale yaliyo machoni penu. Kama mtu yeyote anaamini kuwa yeye ni mali ya Kristo, basi kumbuka kuwa kama ulivyo wa Kristo, vivyo hivyo na sisi ndivyo tulivyo. 8Basi hata kama nikijisifu zaidi kidogo kuhusu mamlaka tuliyo nayo, ambayo Bwana alitupa ili kuwajenga wala si kuwabomoa, mimi sitaionea haya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.