2 Nyakati 8:4
2 Chronicles 8:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pia akajenga mji wa Tadmori katika jangwa na miji yote ya kuhifadhia vitu katika Hamathi.
2 Chronicles 8:4 in English
2 Chronicles 8:4 · Berean Standard Bible
He built Tadmor in the wilderness, in addition to all the store cities that he had built in Hamath.
Context
2Solomoni akajenga tena vijiji vile ambavyo Hiramu alikuwa amempa, naye akawapa Waisraeli waishi humo. 3Kisha Solomoni akaenda Hamath-Soba na kuuteka. 4Pia akajenga mji wa Tadmori katika jangwa na miji yote ya kuhifadhia vitu katika Hamathi. 5Akajenga tena Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, miji yenye ngome, kuta, malango na makomeo. 6Solomoni pia akajenga Baalathi na miji yake yote ya kuhifadhia vitu, na miji kwa ajili ya magari yake na kwa ajili ya farasi wake, chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni na katika nchi yote aliyotawala.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.