Native Bible

2 Chronicles 31:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati Hezekia na maafisa wake walipokuja na kuona yale malundo, wakamsifu Bwana na kuwabariki watu wake Israeli.

2 Chronicles 31:8 in English

2 Chronicles 31:8 · Berean Standard Bible

When Hezekiah and his officials came and viewed the heaps, they blessed the LORD and His people Israel.

Context

6Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda wakaleta pia fungu la kumi la makundi yao ya ngʼombe na makundi ya kondoo na mbuzi pia na fungu la kumi la vitu vitakatifu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya Bwana Mungu wao na kuvikusanya katika malundo. 7Wakaanza kufanya haya katika mwezi wa tatu na kumaliza katika mwezi wa saba. 8Wakati Hezekia na maafisa wake walipokuja na kuona yale malundo, wakamsifu Bwana na kuwabariki watu wake Israeli. 9Hezekia akawauliza makuhani na Walawi kuhusu yale malundo, 10naye Azaria aliyekuwa kuhani mkuu, kutoka jamaa ya Sadoki, akajibu, “Tangu watu walipoanza kuleta sadaka zao katika Hekalu la Bwana tumekuwa na chakula cha kutosha na vingi vya kuweka akiba kwa sababu Bwana amewabariki watu wake, hivyo tumekuwa na kiasi kingi kilichobaki.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.