2 Nyakati 31:7
2 Chronicles 31:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakaanza kufanya haya katika mwezi wa tatu na kumaliza katika mwezi wa saba.
2 Chronicles 31:7 in English
2 Chronicles 31:7 · Berean Standard Bible
In the third month they began building up the heaps, and they finished in the seventh month.
Context
5Mara tu baada ya kutolewa tangazo hilo, Waisraeli wakatoa kwa ukarimu malimbuko ya nafaka zao, divai mpya, mafuta na asali pamoja na vyote vilivyotoka mashambani. Wakaleta kiasi kikubwa cha fungu la kumi la kila kitu. 6Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda wakaleta pia fungu la kumi la makundi yao ya ngʼombe na makundi ya kondoo na mbuzi pia na fungu la kumi la vitu vitakatifu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya Bwana Mungu wao na kuvikusanya katika malundo. 7Wakaanza kufanya haya katika mwezi wa tatu na kumaliza katika mwezi wa saba. 8Wakati Hezekia na maafisa wake walipokuja na kuona yale malundo, wakamsifu Bwana na kuwabariki watu wake Israeli. 9Hezekia akawauliza makuhani na Walawi kuhusu yale malundo,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.