2 Nyakati 3:9
2 Chronicles 3:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Misumari ya dhahabu ilikuwa na uzito wa shekeli hamsini.* Alivifunika pia vyumba vya juu kwa dhahabu.
2 Chronicles 3:9 in English
2 Chronicles 3:9 · Berean Standard Bible
The weight of the nails was fifty shekels of gold.* He also overlaid the upper area with gold.
Context
7Akazifunika boriti za dari, miimo na vizingiti vya milango, kuta na milango ya Hekalu kwa dhahabu, naye akatia nakshi ya makerubi kwenye kuta. 8Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 120* za dhahabu safi. 9Misumari ya dhahabu ilikuwa na uzito wa shekeli hamsini.* Alivifunika pia vyumba vya juu kwa dhahabu. 10Katika sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu akafanyiza jozi moja ya makerubi ya kuchongwa na kuyafunika kwa dhahabu. 11Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano,* nalo liligusa ukuta wa Hekalu, bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi lingine.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.