Native Bible

2 Chronicles 3:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akazifunika boriti za dari, miimo na vizingiti vya milango, kuta na milango ya Hekalu kwa dhahabu, naye akatia nakshi ya makerubi kwenye kuta.

2 Chronicles 3:7 in English

2 Chronicles 3:7 · Berean Standard Bible

He overlaid its beams, thresholds, walls, and doors with gold, and he carved cherubim on the walls.

Context

5Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuupamba kwa miti ya mitende na kuifanyizia kwa minyororo. 6Alilipamba Hekalu kwa vito vya thamani. Hiyo dhahabu aliyotumia ilikuwa dhahabu ya Parvaimu. 7Akazifunika boriti za dari, miimo na vizingiti vya milango, kuta na milango ya Hekalu kwa dhahabu, naye akatia nakshi ya makerubi kwenye kuta. 8Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 120* za dhahabu safi. 9Misumari ya dhahabu ilikuwa na uzito wa shekeli hamsini.* Alivifunika pia vyumba vya juu kwa dhahabu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.