2 Nyakati 24:2
2 Chronicles 24:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana miaka yote ya Yehoyada kuhani.
2 Chronicles 24:2 in English
2 Chronicles 24:2 · Berean Standard Bible
And Joash did what was right in the eyes of the LORD all the days of Jehoiada the priest.
Context
1Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka arobaini. Mama yake aliitwa Sibia aliyekuwa ametoka Beer-Sheba. 2Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana miaka yote ya Yehoyada kuhani. 3Yehoyada akamwoza wake wawili, akazaa watoto wa kiume na wa kike. 4Baada ya muda, Yoashi akaamua kukarabati Hekalu la Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.