Native Bible

2 Chronicles 24:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yehoyada akamwoza wake wawili, akazaa watoto wa kiume na wa kike.

2 Chronicles 24:3 in English

2 Chronicles 24:3 · Berean Standard Bible

Jehoiada took for himself two wives, and he had sons and daughters.

Context

1Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka arobaini. Mama yake aliitwa Sibia aliyekuwa ametoka Beer-Sheba. 2Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana miaka yote ya Yehoyada kuhani. 3Yehoyada akamwoza wake wawili, akazaa watoto wa kiume na wa kike. 4Baada ya muda, Yoashi akaamua kukarabati Hekalu la Bwana. 5Akawaita pamoja makuhani na Walawi akawaambia, “Nendeni katika miji ya Yuda mkakusanye fedha wanazopaswa kulipa kila mwaka kutoka kwa Israeli wote, ili kukarabati Hekalu la Mungu wenu. Fanyeni hivyo sasa.” Lakini Walawi hawakufanya upesi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.