2 Nyakati 24:4
2 Chronicles 24:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada ya muda, Yoashi akaamua kukarabati Hekalu la Bwana.
2 Chronicles 24:4 in English
2 Chronicles 24:4 · Berean Standard Bible
Some time later, Joash set his heart on repairing the house of the LORD.
Context
2Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana miaka yote ya Yehoyada kuhani. 3Yehoyada akamwoza wake wawili, akazaa watoto wa kiume na wa kike. 4Baada ya muda, Yoashi akaamua kukarabati Hekalu la Bwana. 5Akawaita pamoja makuhani na Walawi akawaambia, “Nendeni katika miji ya Yuda mkakusanye fedha wanazopaswa kulipa kila mwaka kutoka kwa Israeli wote, ili kukarabati Hekalu la Mungu wenu. Fanyeni hivyo sasa.” Lakini Walawi hawakufanya upesi. 6Kwa hiyo mfalme akamwita Yehoyada kuhani mkuu na kumwambia, “Kwa nini hukuwaambia Walawi walete kutoka Yuda na Yerusalemu kodi iliyowekwa na Mose mtumishi wa Bwana pamoja na kusanyiko la Israeli kwa ajili ya Hema ya Ushuhuda?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.