Native Bible

2 Chronicles 2:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitawapa watumishi wako, yaani, maseremala wakatao mbao, kori 20,000* za unga wa ngano, kori 20,000 za shayiri, bathi 20,000* za mvinyo, na bathi 20,000 za mafuta ya zeituni.”

2 Chronicles 2:10 in English

2 Chronicles 2:10 · Berean Standard Bible

I will pay your servants, the woodcutters, 20,000 cors of ground wheat,* 20,000 cors of barley,* 20,000 baths of wine,* and 20,000 baths of olive oil.*”

Context

8“Pia nitumie magogo ya mierezi, miberoshi na misandali kutoka Lebanoni kwa maana najua kwamba watu wako wanao ujuzi wa kupasua mbao huko. Watu wangu watafanya kazi pamoja na watu wako 9ili wanipatie mbao kwa wingi kwa sababu Hekalu nitakalojenga lazima liwe kubwa na zuri kabisa. 10Nitawapa watumishi wako, yaani, maseremala wakatao mbao, kori 20,000* za unga wa ngano, kori 20,000 za shayiri, bathi 20,000* za mvinyo, na bathi 20,000 za mafuta ya zeituni.” 11Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akamjibu Solomoni kwa barua: “Kwa sababu Bwana anawapenda watu wake, amekufanya wewe kuwa mfalme wao.” 12Naye Hiramu akaongeza kusema: “Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli aliyezifanya mbingu na nchi! Amempa Mfalme Daudi mwana mwenye hekima, aliyejaliwa maarifa na ufahamu, ambaye atajenga Hekalu kwa ajili ya Bwana, na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.