2 Nyakati 2:11
2 Chronicles 2:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akamjibu Solomoni kwa barua: “Kwa sababu Bwana anawapenda watu wake, amekufanya wewe kuwa mfalme wao.”
2 Chronicles 2:11 in English
2 Chronicles 2:11 · Berean Standard Bible
Then Hiram king of Tyre wrote a letter in reply to Solomon: “Because the LORD loves His people, He has set you over them as king.”
Context
9ili wanipatie mbao kwa wingi kwa sababu Hekalu nitakalojenga lazima liwe kubwa na zuri kabisa. 10Nitawapa watumishi wako, yaani, maseremala wakatao mbao, kori 20,000* za unga wa ngano, kori 20,000 za shayiri, bathi 20,000* za mvinyo, na bathi 20,000 za mafuta ya zeituni.” 11Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akamjibu Solomoni kwa barua:
“Kwa sababu Bwana anawapenda watu wake, amekufanya wewe kuwa mfalme wao.” 12Naye Hiramu akaongeza kusema:
“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli aliyezifanya mbingu na nchi! Amempa Mfalme Daudi mwana mwenye hekima, aliyejaliwa maarifa na ufahamu, ambaye atajenga Hekalu kwa ajili ya Bwana, na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe. 13“Mimi nitamtuma kwako Huramu-Abi, mtu mwenye ustadi mwingi,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.