Native Bible

2 Chronicles 2:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

ili wanipatie mbao kwa wingi kwa sababu Hekalu nitakalojenga lazima liwe kubwa na zuri kabisa.

2 Chronicles 2:9 in English

2 Chronicles 2:9 · Berean Standard Bible

to prepare for me timber in abundance, because the temple I am building will be great and wonderful.

Context

7“Hivyo basi nitumie mtu mwenye ustadi wa kufanya kazi ya kutengeneza dhahabu na fedha, shaba na chuma, nyuzi za rangi ya zambarau, nyekundu na buluu, mwenye uzoefu wa kutia nakshi, ili afanye kazi Yuda na Yerusalemu pamoja na mafundi wangu wenye ustadi, ambao baba yangu Daudi aliwaweka. 8“Pia nitumie magogo ya mierezi, miberoshi na misandali kutoka Lebanoni kwa maana najua kwamba watu wako wanao ujuzi wa kupasua mbao huko. Watu wangu watafanya kazi pamoja na watu wako 9ili wanipatie mbao kwa wingi kwa sababu Hekalu nitakalojenga lazima liwe kubwa na zuri kabisa. 10Nitawapa watumishi wako, yaani, maseremala wakatao mbao, kori 20,000* za unga wa ngano, kori 20,000 za shayiri, bathi 20,000* za mvinyo, na bathi 20,000 za mafuta ya zeituni.” 11Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akamjibu Solomoni kwa barua: “Kwa sababu Bwana anawapenda watu wake, amekufanya wewe kuwa mfalme wao.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.