Native Bible

2 Chronicles 13:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Abiya na watu wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi 500,000 miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli.

2 Chronicles 13:17 in English

2 Chronicles 13:17 · Berean Standard Bible

Then Abijah and his people struck them with a mighty blow, and 500,000 chosen men of Israel fell slain.

Context

15nao watu wa Yuda wakapaza sauti ya kilio cha vita. Katika kupiga kelele za vita, Mungu akawafukuza Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Mfalme Abiya na Yuda. 16Waisraeli wakakimbia mbele ya Yuda, naye Mungu akawatia Israeli mikononi mwao. 17Abiya na watu wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi 500,000 miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli. 18Watu wa Israeli walitiishwa katika tukio lile, nao watu wa Yuda wakawa washindi kwa sababu walimtegemea Bwana, Mungu wa baba zao. 19Abiya akamfuatia Yeroboamu na kuteka miji ya Betheli, Yeshana na Efroni kutoka kwake, pamoja na vijiji vinavyoizunguka miji hiyo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.