2 Nyakati 13:16
2 Chronicles 13:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waisraeli wakakimbia mbele ya Yuda, naye Mungu akawatia Israeli mikononi mwao.
2 Chronicles 13:16 in English
2 Chronicles 13:16 · Berean Standard Bible
So the Israelites fled before Judah, and God delivered them into their hands.
Context
14Basi Yuda wakageuka na kuona kwamba wanashambuliwa mbele na nyuma. Ndipo wakamlilia Bwana. Makuhani wakapiga tarumbeta zao, 15nao watu wa Yuda wakapaza sauti ya kilio cha vita. Katika kupiga kelele za vita, Mungu akawafukuza Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Mfalme Abiya na Yuda. 16Waisraeli wakakimbia mbele ya Yuda, naye Mungu akawatia Israeli mikononi mwao. 17Abiya na watu wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi 500,000 miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli. 18Watu wa Israeli walitiishwa katika tukio lile, nao watu wa Yuda wakawa washindi kwa sababu walimtegemea Bwana, Mungu wa baba zao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.