1 Timotheo 5:6
1 Timothy 5:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini mjane aishiye kwa anasa amekufa, ingawa anaishi.
1 Timothy 5:6 in English
1 Timothy 5:6 · Berean Standard Bible
But she who lives for pleasure is dead even while she is still alive.
Context
4Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hawa inawapasa awali ya yote wajifunze kutimiza wajibu wao wa kumcha Mungu katika matendo kwa kuwatunza wale wa jamaa zao wenyewe, na hivyo wawarudishie wema waliowatendea wazazi wao, kwa kuwa hivi ndivyo impendezavyo Mungu. 5Mwanamke ambaye ni mjane kweli kweli, yaani, yeye aliyebaki peke yake huweka tumaini lake kwa Mungu naye hudumu katika maombi usiku na mchana akimwomba Mungu ili amsaidie. 6Lakini mjane aishiye kwa anasa amekufa, ingawa anaishi. 7Wape watu maagizo haya pia, ili asiwepo yeyote wa kulaumiwa. 8Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.