Native Bible

1 Timothy 5:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.

1 Timothy 5:8 in English

1 Timothy 5:8 · Berean Standard Bible

If anyone does not provide for his own, and especially his own household, he has denied the faith and is worse than an unbeliever.

Context

6Lakini mjane aishiye kwa anasa amekufa, ingawa anaishi. 7Wape watu maagizo haya pia, ili asiwepo yeyote wa kulaumiwa. 8Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini. 9Mjane yeyote asiwekwe kwenye orodha ya wajane isipokuwa awe ametimiza umri wa miaka sitini, na ambaye alikuwa mke wa mume mmoja, 10awe ameshuhudiwa kwa matendo yake mema, aliyewalea watoto wake vizuri, aliye mkarimu, aliyewanawisha watakatifu miguu, aliyewasaidia wenye shida na aliyejitolea kwa ajili ya matendo mema ya kila namna.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.