1 Timotheo 2:3
1 Timothy 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu,
1 Timothy 2:3 in English
1 Timothy 2:3 · Berean Standard Bible
This is good and pleasing in the sight of God our Savior,
Context
1Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: 2kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. 3Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu, 4anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli. 5Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.