1 Wathesalonike 5:13
1 Thessalonians 5:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waheshimuni sana katika upendo kwa ajili ya kazi zao. Ishini kwa amani ninyi kwa ninyi.
1 Thessalonians 5:13 in English
1 Thessalonians 5:13 · Berean Standard Bible
In love, hold them in highest regard because of their work. Live in peace with one another.
Context
11Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa. 12Sasa tunawaomba, ndugu, waheshimuni wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu, wale ambao wana mamlaka juu yenu katika Bwana na ambao wanawaonya. 13Waheshimuni sana katika upendo kwa ajili ya kazi zao. Ishini kwa amani ninyi kwa ninyi. 14Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni walio wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na kuwavumilia watu wote. 15Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.