1 Samweli 20:39
1 Samuel 20:39 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
(Mvulana hakujua chochote juu ya hayo yote; Yonathani na Daudi tu ndio waliojua.)
1 Samuel 20:39 in English
1 Samuel 20:39 · Berean Standard Bible
But the boy did not know anything; only Jonathan and David knew the arrangement.
Context
37Yule mvulana alipofika mahali pale ambapo mshale wa Yonathani ulipokuwa umeanguka, Yonathani akamwita, “Je, mshale hauko mbele yako?” 38Yonathani akampigia kelele, “Harakisha, nenda haraka! Usisimame!” Mvulana akaokota mshale na kurudi kwa bwana wake. 39(Mvulana hakujua chochote juu ya hayo yote; Yonathani na Daudi tu ndio waliojua.) 40Basi Yonathani akampa yule mvulana silaha zake na kumwambia, “Nenda, zirudishe mjini.” 41Baada ya mvulana kwenda, Daudi akainuka kutoka upande wa kusini wa lile jiwe, naye akasujudu uso wake mpaka nchi mara tatu mbele ya Yonathani. Kisha kila mmoja akambusu mwenzake, wakalia pamoja. Lakini Daudi akalia zaidi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.