1 Samweli 20:40
1 Samuel 20:40 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi Yonathani akampa yule mvulana silaha zake na kumwambia, “Nenda, zirudishe mjini.”
1 Samuel 20:40 in English
1 Samuel 20:40 · Berean Standard Bible
Then Jonathan gave his equipment to the boy and said, “Go, take it back to the city.”
Context
38Yonathani akampigia kelele, “Harakisha, nenda haraka! Usisimame!” Mvulana akaokota mshale na kurudi kwa bwana wake. 39(Mvulana hakujua chochote juu ya hayo yote; Yonathani na Daudi tu ndio waliojua.) 40Basi Yonathani akampa yule mvulana silaha zake na kumwambia, “Nenda, zirudishe mjini.” 41Baada ya mvulana kwenda, Daudi akainuka kutoka upande wa kusini wa lile jiwe, naye akasujudu uso wake mpaka nchi mara tatu mbele ya Yonathani. Kisha kila mmoja akambusu mwenzake, wakalia pamoja. Lakini Daudi akalia zaidi. 42Yonathani akamwambia Daudi, “Nenda kwa amani, kwa kuwa tumeapiana kiapo cha urafiki kati yetu kwa jina la Bwana, tukisema, ‘Bwana ndiye shahidi kati yako na mimi, na kati ya wazao wako na wazao wangu milele.’ ” Kisha Daudi akaondoka, naye Yonathani akarudi mjini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.