1 Samweli 19:13
1 Samuel 19:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Mikali akachukua kinyago, akakilaza kitandani, akakifunika kwa vazi na kukiwekea singa za mbuzi kichwani.
1 Samuel 19:13 in English
1 Samuel 19:13 · Berean Standard Bible
Then Michal took a household idol * and laid it in the bed, placed some goat hair on its head, and covered it with a garment.
Context
11Sauli akatuma watu nyumbani mwa Daudi wailinde hiyo nyumba na kumuua asubuhi. Lakini Mikali, mkewe Daudi, akamwonya akisema, “Kama hukukimbia kuokoa maisha yako usiku huu, kesho yake utauawa.” 12Basi Mikali akamteremsha Daudi kupitia dirishani, naye akakimbia na kuokoka. 13Kisha Mikali akachukua kinyago, akakilaza kitandani, akakifunika kwa vazi na kukiwekea singa za mbuzi kichwani. 14Sauli alipotuma watu kumkamata Daudi, Mikali akasema, “Yeye ni mgonjwa.” 15Kisha Sauli akatuma watu tena kumwona Daudi naye akawaambia, “Mleteni kwangu juu ya kitanda chake ili nipate kumuua.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.