Native Bible

1 Samuel 19:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha Sauli akatuma watu tena kumwona Daudi naye akawaambia, “Mleteni kwangu juu ya kitanda chake ili nipate kumuua.”

1 Samuel 19:15 in English

1 Samuel 19:15 · Berean Standard Bible

But Saul sent the messengers back to see David and told them, “Bring him up to me in his bed so I can kill him.”

Context

13Kisha Mikali akachukua kinyago, akakilaza kitandani, akakifunika kwa vazi na kukiwekea singa za mbuzi kichwani. 14Sauli alipotuma watu kumkamata Daudi, Mikali akasema, “Yeye ni mgonjwa.” 15Kisha Sauli akatuma watu tena kumwona Daudi naye akawaambia, “Mleteni kwangu juu ya kitanda chake ili nipate kumuua.” 16Lakini wale watu walipoingia, kumbe ni kinyago tu kilichokuwa kitandani na kwenye kichwa kulikuwepo na singa za mbuzi. 17Sauli akamwambia Mikali, “Kwa nini umenidanganya mimi hivi na kumwacha adui yangu aende zake ili apate kuokoka?” Mikali akamwambia, “Yeye aliniambia, ‘Niache niende zangu. Kwa nini nikuue?’ ”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.