1 Samweli 16:10
1 Samuel 16:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yese alikuwa na wana saba aliowapitisha mbele ya Samweli, lakini Samweli akamwambia, “Bwana hajawachagua hawa.”
1 Samuel 16:10 in English
1 Samuel 16:10 · Berean Standard Bible
Thus Jesse made seven of his sons pass before Samuel, but Samuel told him, “The LORD has not chosen any of these.”
Context
8Kisha Yese akamwita Abinadabu na kumpitisha mbele ya Samweli. Lakini Samweli akasema, “Hata huyu Bwana hakumchagua.” 9Kisha Yese akampitisha Shama, lakini Samweli akasema, “Wala huyu Bwana hakumchagua.” 10Yese alikuwa na wana saba aliowapitisha mbele ya Samweli, lakini Samweli akamwambia, “Bwana hajawachagua hawa.” 11Hivyo akamuuliza Yese, “Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?”
Yese akajibu, “Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo.”
Samweli akasema, “Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike.” 12Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.
Ndipo Bwana akasema, “Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.