1 Samweli 16:12
1 Samuel 16:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza. Ndipo Bwana akasema, “Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye.”
1 Samuel 16:12 in English
1 Samuel 16:12 · Berean Standard Bible
So Jesse sent for his youngest son and brought him in. He was ruddy, with beautiful eyes and a handsome appearance. And the LORD said, “Rise and anoint him, for he is the one.”
Context
10Yese alikuwa na wana saba aliowapitisha mbele ya Samweli, lakini Samweli akamwambia, “Bwana hajawachagua hawa.” 11Hivyo akamuuliza Yese, “Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?”
Yese akajibu, “Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo.”
Samweli akasema, “Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike.” 12Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.
Ndipo Bwana akasema, “Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye.” 13Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa Bwana akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama. 14Basi Roho wa Bwana alikuwa ameondoka kwa Sauli, nayo roho mbaya ikaachiwa nafasi na Bwana ili imtese.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.