1 Samweli 16:11
1 Samuel 16:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo akamuuliza Yese, “Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?” Yese akajibu, “Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo.” Samweli akasema, “Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike.”
1 Samuel 16:11 in English
1 Samuel 16:11 · Berean Standard Bible
And Samuel asked him, “Are these all the sons you have?” “There is still the youngest,” Jesse replied, “but he is tending the sheep.” “Send for him,” Samuel replied. “For we will not sit down to eat until he arrives.”
Context
9Kisha Yese akampitisha Shama, lakini Samweli akasema, “Wala huyu Bwana hakumchagua.” 10Yese alikuwa na wana saba aliowapitisha mbele ya Samweli, lakini Samweli akamwambia, “Bwana hajawachagua hawa.” 11Hivyo akamuuliza Yese, “Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?”
Yese akajibu, “Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo.”
Samweli akasema, “Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike.” 12Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.
Ndipo Bwana akasema, “Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye.” 13Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa Bwana akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.