1 Samweli 10:21
1 Samuel 10:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha akalisogeza mbele kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo, nao ukoo wa Matri ukachaguliwa. Mwishoni Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipomtafuta, hakuonekana.
1 Samuel 10:21 in English
1 Samuel 10:21 · Berean Standard Bible
Then he had the tribe of Benjamin come forward by its clans, and the clan of Matri was selected.* Finally, Saul son of Kish was selected. But when they looked for him, they could not find him.
Context
19Lakini sasa mmemkataa Mungu wenu, ambaye anawaokoa toka katika maafa yenu yote na taabu zenu zote. Nanyi mmesema, ‘Hapana, tuteulie mfalme atutawale.’ Sasa basi, jihudhurisheni wenyewe mbele za Bwana kwa kabila zenu na kwa koo zenu.” 20Samweli alipoyasogeza makabila yote ya Israeli, kabila la Benyamini likachaguliwa. 21Kisha akalisogeza mbele kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo, nao ukoo wa Matri ukachaguliwa. Mwishoni Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipomtafuta, hakuonekana. 22Wakazidi kuuliza kwa Bwana, “Je, huyo mtu amekwisha kufika hapa?”
Naye Bwana akasema, “Ndiyo, amejificha katikati ya mizigo.” 23Wakakimbia na kumleta kutoka huko, naye aliposimama katikati ya watu, alikuwa mrefu kuliko watu wengine wote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.