1 Petro 4:8
1 Peter 4:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi.
1 Peter 4:8 in English
1 Peter 4:8 · Berean Standard Bible
Above all, love one another deeply, because love covers over a multitude of sins.*
Context
6Kwa kuwa hii ndiyo sababu Injili ilihubiriwa hata kwa wale waliokufa, ili wahukumiwe sawasawa na wanadamu wengine katika mwili, lakini katika roho waishi kulingana na Mungu aishivyo. 7Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo kuweni na akili tulivu na kiasi, mkikesha katika kuomba. 8Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi. 9Kuweni wakarimu kila mtu na mwenzake pasipo manungʼuniko. 10Kila mmoja na atumie kipawa chochote alichopewa kuwahudumia wengine, kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.