1 Petro 4:9
1 Peter 4:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kuweni wakarimu kila mtu na mwenzake pasipo manungʼuniko.
1 Peter 4:9 in English
1 Peter 4:9 · Berean Standard Bible
Show hospitality to one another without complaining.
Context
7Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo kuweni na akili tulivu na kiasi, mkikesha katika kuomba. 8Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi. 9Kuweni wakarimu kila mtu na mwenzake pasipo manungʼuniko. 10Kila mmoja na atumie kipawa chochote alichopewa kuwahudumia wengine, kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu. 11Yeyote asemaye hana budi kusema kama mtu asemaye maneno ya Mungu mwenyewe. Yeyote ahudumuye hana budi kuhudumu kwa nguvu zile anazopewa na Mungu, ili Mungu apate kutukuzwa katika mambo yote kwa njia ya Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye milele na milele. Amen.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.