Native Bible

1 Peter 3:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa maana, “Yeyote apendaye uzima na kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila.

1 Peter 3:10 in English

1 Peter 3:10 · Berean Standard Bible

For, “Whoever would love life and see good days must keep his tongue from evil and his lips from deceitful speech.

Context

8Hatimaye, ninyi nyote kuweni na nia moja, wenye kuhurumiana, mkipendana kama ndugu, na mwe wasikitivu na wanyenyekevu. 9Msilipe ovu kwa ovu, au jeuri kwa jeuri, bali barikini, kwa maana hili ndilo mliloitiwa ili mpate kurithi baraka. 10Kwa maana, “Yeyote apendaye uzima na kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila. 11Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema; lazima aitafute amani na kuifuatilia sana. 12Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza maombi yao. Bali uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.