Native Bible

1 Kings 9:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mfalme Solomoni pia akatengeneza pia meli huko Esion-Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika Edomu, kwenye ukingo wa Bahari ya Shamu.*

1 Kings 9:26 in English

1 Kings 9:26 · Berean Standard Bible

King Solomon also assembled a fleet of ships at Ezion-geber, which is near Eloth * in Edom, on the shore of the Red Sea.*

Context

24Baada ya binti Farao kuja kutoka Mji wa Daudi na kuingia jumba la kifalme ambalo Solomoni alikuwa amemjengea, akajenga Milo. 25Solomoni akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani mara tatu kwa mwaka, juu ya madhabahu aliyokuwa amejengea kwa ajili ya Bwana, akifukiza uvumba mbele za Bwana pamoja na dhabihu hizo, hivyo kutimiza kanuni za hekalu. 26Mfalme Solomoni pia akatengeneza pia meli huko Esion-Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika Edomu, kwenye ukingo wa Bahari ya Shamu.* 27Naye Hiramu akawatuma watu wake; mabaharia walioijua bahari, kuhudumu katika hizo meli pamoja na watu wa Solomoni. 28Wakasafiri kwa bahari mpaka Ofiri na kurudi na talanta 420* za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Solomoni.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.