Native Bible

1 Kings 6:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akatengeneza madirisha membamba yenye vidirisha vidogo vya juu katika Hekalu.

1 Kings 6:4 in English

1 Kings 6:4 · Berean Standard Bible

He also had narrow windows framed high in the temple.

Context

2Hekalu hilo Mfalme Solomoni alilojenga kwa ajili ya Bwana lilikuwa na urefu wa dhiraa sitini,* upana wa dhiraa ishirini* na kimo cha dhiraa thelathini* kwenda juu. 3Baraza ya mbele ya Hekalu ilienea dhiraa ishirini kulingana na upana wa Hekalu na kujitokeza dhiraa kumi mbele ya Hekalu. 4Akatengeneza madirisha membamba yenye vidirisha vidogo vya juu katika Hekalu. 5Akafanyiza vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote vikishikamana na kuta za Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu. 6Ghorofa ya chini kabisa ilikuwa na upana wa dhiraa tano,* ya kati ilikuwa dhiraa sita na ya tatu ilikuwa dhiraa saba.* Kuzunguka ukuta wa nje wa Hekalu akapunguza ukuta pande zote ili boriti zisishikane kwenye kuta za Hekalu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.