1 Wafalme 6:3
1 Kings 6:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baraza ya mbele ya Hekalu ilienea dhiraa ishirini kulingana na upana wa Hekalu na kujitokeza dhiraa kumi mbele ya Hekalu.
1 Kings 6:3 in English
1 Kings 6:3 · Berean Standard Bible
The portico at the front of the main hall of the temple was twenty cubits * long, extending across the width of the temple and projecting out ten cubits * in front of the temple.
Context
1Katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Solomoni katika Israeli, katika mwezi wa Zivu, ambao ndio mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la Bwana. 2Hekalu hilo Mfalme Solomoni alilojenga kwa ajili ya Bwana lilikuwa na urefu wa dhiraa sitini,* upana wa dhiraa ishirini* na kimo cha dhiraa thelathini* kwenda juu. 3Baraza ya mbele ya Hekalu ilienea dhiraa ishirini kulingana na upana wa Hekalu na kujitokeza dhiraa kumi mbele ya Hekalu. 4Akatengeneza madirisha membamba yenye vidirisha vidogo vya juu katika Hekalu. 5Akafanyiza vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote vikishikamana na kuta za Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.