1 Wafalme 6:6
1 Kings 6:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ghorofa ya chini kabisa ilikuwa na upana wa dhiraa tano,* ya kati ilikuwa dhiraa sita na ya tatu ilikuwa dhiraa saba.* Kuzunguka ukuta wa nje wa Hekalu akapunguza ukuta pande zote ili boriti zisishikane kwenye kuta za Hekalu.
1 Kings 6:6 in English
1 Kings 6:6 · Berean Standard Bible
The bottom floor was five cubits wide,* the middle floor six cubits,* and the third floor seven cubits.* He also placed offset ledges around the outside of the temple, so that nothing would be inserted into its walls.
Context
4Akatengeneza madirisha membamba yenye vidirisha vidogo vya juu katika Hekalu. 5Akafanyiza vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote vikishikamana na kuta za Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu. 6Ghorofa ya chini kabisa ilikuwa na upana wa dhiraa tano,* ya kati ilikuwa dhiraa sita na ya tatu ilikuwa dhiraa saba.* Kuzunguka ukuta wa nje wa Hekalu akapunguza ukuta pande zote ili boriti zisishikane kwenye kuta za Hekalu. 7Katika kujenga Hekalu, yalitumika tu mawe yaliyochongwa huko machimboni, wala hakuna nyundo, patasi au chombo kingine chochote cha chuma kilichosikika sauti yake katika eneo la ujenzi wa Hekalu wakati lilipokuwa likijengwa. 8Ingilio la ghorofa ya chini kabisa lilikuwa upande wa kusini wa Hekalu, ngazi ilielekea ghorofa ya kati na kutokea hapo ilielekea hadi ghorofa ya tatu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.