Native Bible

1 Kings 3:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Siku ya tatu baada ya mtoto wangu kuzaliwa, mwanamke huyu pia naye akazaa mtoto. Tulikuwa peke yetu, hapakuwa na mtu mwingine yeyote katika nyumba isipokuwa sisi wawili.

1 Kings 3:18 in English

1 Kings 3:18 · Berean Standard Bible

On the third day after I gave birth, this woman also had a baby. We were alone, with no one in the house but the two of us.

Context

16Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake. 17Mmojawapo akasema, “Bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunaishi kwenye nyumba moja. Nilikuwa nimezaa alipokuwa pamoja nami. 18Siku ya tatu baada ya mtoto wangu kuzaliwa, mwanamke huyu pia naye akazaa mtoto. Tulikuwa peke yetu, hapakuwa na mtu mwingine yeyote katika nyumba isipokuwa sisi wawili. 19“Wakati wa usiku mwana wa huyu mwanamke akafa kwa sababu alimlalia. 20Hivyo akaondoka katikati ya usiku na kumchukua mwanangu kutoka ubavuni pangu wakati mimi mtumishi wako nilipokuwa nimelala. Akamweka kifuani mwake na kumweka mwanawe aliyekufa kifuani mwangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.