Native Bible

1 Kings 3:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mmojawapo akasema, “Bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunaishi kwenye nyumba moja. Nilikuwa nimezaa alipokuwa pamoja nami.

1 Kings 3:17 in English

1 Kings 3:17 · Berean Standard Bible

One woman said, “Please, my lord, this woman and I live in the same house, and I gave birth while she was in the house.

Context

15Ndipo Solomoni akaamka, akatambua kuwa ilikuwa ndoto. Akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya Sanduku la Agano la Bwana, naye akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha akawafanyia watumishi wake wote karamu. 16Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake. 17Mmojawapo akasema, “Bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunaishi kwenye nyumba moja. Nilikuwa nimezaa alipokuwa pamoja nami. 18Siku ya tatu baada ya mtoto wangu kuzaliwa, mwanamke huyu pia naye akazaa mtoto. Tulikuwa peke yetu, hapakuwa na mtu mwingine yeyote katika nyumba isipokuwa sisi wawili. 19“Wakati wa usiku mwana wa huyu mwanamke akafa kwa sababu alimlalia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.