1 Wafalme 3:16
1 Kings 3:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake.
1 Kings 3:16 in English
1 Kings 3:16 · Berean Standard Bible
At that time two prostitutes came to the king and stood before him.
Context
14Nawe kama ukienenda katika njia zangu na kutii sheria na amri zangu kama baba yako Daudi alivyofanya, nitakupa maisha marefu.” 15Ndipo Solomoni akaamka, akatambua kuwa ilikuwa ndoto.
Akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya Sanduku la Agano la Bwana, naye akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha akawafanyia watumishi wake wote karamu. 16Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake. 17Mmojawapo akasema, “Bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunaishi kwenye nyumba moja. Nilikuwa nimezaa alipokuwa pamoja nami. 18Siku ya tatu baada ya mtoto wangu kuzaliwa, mwanamke huyu pia naye akazaa mtoto. Tulikuwa peke yetu, hapakuwa na mtu mwingine yeyote katika nyumba isipokuwa sisi wawili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.